The House of Favourite Newspapers

Kopa, Chocky Kufunika Valentine Dar Live

0

AllyChokinewAli Chocky

Mwandishi Wetu, RISASI

ZIKIWA zimesalia siku tatu tu kufikia Februari 14, (Valentine’s Day), mastaa wa Muziki wa Dansi na Taarab, Ali Chocky, Khadija Kopa pamoja na Hassan Bitchuka wanatarajiwa kufunika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem ambapo kutakuwa na usiku wa muziki mtamu wa wakongwe.
Siku hiyo ambayo ni maalum kwa wapendanao, itawakutanisha wakongwe wa Muziki wa Dansi ambao ni The African Stars ‘Twanga Pepeta’ Sikinde, Msondo Ngoma pamoja na Kundi la Muziki wa Taarab, TOT chini ya Khadija Kopa.

khadija_kopa1Khadija Kopa

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo aliwaomba wapendanao kujitokeza kwa wingi kuja kupata raha ya muziki ambayo itawakumbusha mbali.

“Itakuwa ni historia kwa wapendanao kwani kwa mara ya kwanza bendi hizi kongwe zitakutana Dar Live Siku ya Wapendanao kutoa ladha ya aina yake. Na niwaahidi kwa wote watakaopendeza, Dar Live imewaandalia zawadi maalum,” alisema Mbizo na kuongezea kuwa kiingilio kitakuwa ni Sh. 20,000 tu kwa VIP na kawaida Sh. 10,000.

Leave A Reply