The House of Favourite Newspapers

Mawakili Kesi ya kigogo Wa Milioni 7 Watoana Jasho Mahakamani

0

IMG_0806

Yusufali na mwenzake wakibadilishana mawazo, kabla ya kuanza kunguruma kwa kesi inayowakabili.

IMG_0807

Wanasheria, waandishi wa habari na ndugu wa washtakiwa wakiwa mahakamani hapo.

Kesi inayomkabili mfanyabiashara Mohamed Mustafa Yusufali anayedaiwa kujiingia fedha zipatazo shilingi milioni saba kwa dakika kwa njia isiyo halali, leo imechukua sura mpya kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar huku mawakili wa pande zote mbili, wakihenyeshana kwa hoja.

Yusufali na wenzake, wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali, yakiwemo udanganyifu, kughushi, kukweka kulipa kodi na kutakatisha fedha haramu pamoja na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 15.6.

Mawakili wa upande wa mshtakiwa, wanaiomba mahakama kumfutia mteja wao shitaka la kutakatisha fedha haramu kwa sababu ya mapungufu yaliyopo kwenye hati ya mashtaka, wakati mawakili wa serikali wanasisitiza kwamba hakuna makosa yaliyofanyika.

Mvutano huo umesababisha kuahirishwa tena kwa kesi hiyo mpaka Agosti 10, mwaka huu itakaposikilizwa tena.

Habari/Picha: Hashim Aziz/ GPL

Leave A Reply