The House of Favourite Newspapers

Mbali na Kumshusha Kocha Mzambia, Yanga Yamleta CEO Mpya

rudouf-2Klabu ya Dar es Salaam Young Africans ‘Yanga’ imeendelea kuchukua vichwa vya habari kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari hapa nchini.

Hii mpya umeipata? Ukiachana na headlines za uongozi wa klabu hiyo kudaiwa kumleta kocha mpya katika klabu hiyo, George Lwandamina kutoka Zesco United ya Zambia taarifa mpya zimetoka Yanga wamemteua mfaransa Jerome Dufourg kuwa afisa mtendaji mkuu (CEO) wa klabu hiyo.

rudouf-1Yanga wameripotiwa kumpa nafasi hiyo Jerome Dufourg ambaye ni mtaalam wa sports business kufuatia mwenyekiti wao Yusuph Manji kudai kuwa Yanga ilipata hasara ya zaidi ya Tsh bilioni 1.5 kwa mwaka jana, Dufourg anatajwa kupewa majukumu ya kuendesha shughuli za klabu hiyo na mipango ya fedha.

Muda wowote kutokea sasa Jerome Dufourg atawasili Tanzania lakini kazi ataanza rasmi Novemba 19, 2016, Dufourg amewahi kufanya kazi na shirikisho la soka la Rwanda pamoja na klabu ya FC Talanta ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Kenya.

Comments are closed.