The House of Favourite Newspapers

Mke Amuua Mumewe kwa Kumzuia Kuondoka Nyumbani

0

 

POLISI katika mji wa Nakuru nchini Kenya wanamshikilia mwanamke mmoja, Rehema Rita Wanjiru, mwenye umri wa miaka 21 kwa tuhuma za kumpiga na kumuua mumewe,  Kevin Kuria, katika eneo la Gorofa Estate.

 

Wanjiru anadaiwa kumchoma kisu kwenye kifua mumewe huyo mwenye umri wa miaka 23 wakati akiwa anajaribu kumzuia kutoka nyumbani kwao asubuhi. Taarifa zinaeleza kuwa Wanjiru alikuwa akibeba vitu vyake kwa lengo la kutaka kuondoka kufuatia mapigano ya mara kwa mara  na mumewe hapo nyumbani kwao.

 

Mjumbe wa nyumba kumi alisema: “Bi Wanjiru alikuwa amebeba koti lake tayari kwa kuondoka lakini mwanaume huyo hakumruhusu aondoke, ndipo ambapo ugomvi ukaibuka, nilipopigiwa simu ili kuja kuamua ugomvi huo nilimkuta mtu huyo amelala chini huku damu zikitiririka kutoka katika kifua chake,” amesema.

 

 

Sambamba na hilo, Mjumbe mwingine wa nyumba kumi,Peter Ng’anganyika,  alisema alimkuta mwanamke huyo akijutia kufanya tukio hilo huku akiwa amekaa karibu na mwili wa mume wake na kupiga simu kwa majirani wamsaidie mumewe apelekwe hospitali.

 

Majirani walisema wanandoa hao mara nyingi walikuwa wakipigana mara kwa mara na kila wakati mwanamke huyo alikuwa akitishia kumuua mumewe.

 

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nakuru, Stephen Matu,  alisema mwili wa mwanaume huyo umepelekwa mochwari ya Hospitali ya Nakuru wakati mtuhumiwa huyo akifikishwa katika kituo cha polisi.

 

Leave A Reply