The House of Favourite Newspapers

Mshindi Wa Shinda Nyumba Awasili Dar Jana (Video Ipo Hapa)

0

1

Mshindi wa Shindano la Shinda Nyumba ,  Nelly Mwangosi  akishuka katika basi Ubungo  jijini Dar jana.

2 (2)

Nelly akipokelewa kwa furaha na ndugu zake.

2

Nelly (aliyeshika maua) akiwa na mumewe (kushoto), mtoto wao (mbele) pamoja na ndugu waliokuja kuwapokea.

3

…Akiwa na familia yake.

5

Ndugu wa mshindi wakiwa na mtoto wa mshindi Ubungo.

6

Nelly Mwangosi akifanya mahojiano na  Global TV Online.

Mshindi wa Shindano la Shinda Nyumba lililokuwa likiendeshwa na Kampuni ya Global Publishers inayochapisha magazeti ya Championi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Uwazi, Nelly Mwangosi  amewasili jana jijini Dar akitokea mkoani Iringa kwa ajili ya kukabidhiwa mjengo huo leo.

Akizungumza katika stendi ya mkoa, Ubungo, Nelly aliyekuwa ameambatana na mumewe na mtoto alisema amefurahi sana kupata ushindi huo na alipopigiwa simu kitu cha kwanza alipiga magoti na kumshukuru Mungu hivyo anawashauri watu wengine wayasome magazeti ya Global na hata kukiwa na shindano washiriki kwani zawadi zinatolewa kweli kabisa siyo uongo.

“Nawashauri watu wayasome sana magazeti ya Global maana mimi nimekuwa nikiyasoma kwa miaka kumi na nane sasa pia linapokuja suala la shindano nawaomba washiriki kwa sababu zawadi zinazotolewa ni kweli na siyo uongo, nitaendelea kuyasoma na ninayaamini sana,” alisema Nelly.

Nelly aliibuka mshindi katika droo ya mwisho iliyochezeshwa Mbagala Zakhem, Dar Juni 30, mwaka huu ambapo kesho atakabidhiwa mjengo wenye thamani ya mamilioni uliopo Salasala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

(HABARI/PICHA: GLADNESS MALLYA/GPL)

Leave A Reply