The House of Favourite Newspapers

Mtangazaji wa The Playlist ya Times FM Kurusha MTV MAMA Live leo

 lil-ommy-2

MTANGAZAJI maarufu wa Kipindi cha The Playlist kinachoruka kupitia Kituo cha Redio cha 100.5 Times FM, Omary Tambwe ‘Lil Ommy’ kwa mara ya kwanza leo anatarajiwa kuripoti live tukio la Utolewaji Tuzo za MAMA’s (Mtv Africa Music Awards 2016) zitakazofanyika leo mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Akizungumza na mtandao huu moja kwa moja kutoka Afrika Kusini, Ommy aliyewahi kufanya mahojiano katika kipindi chake na mastaa kibao wakiwemo, Diamond, AY, Salama Jabir, Idris Sultan na mastaa wengine wa Bongo, Nigeria, Kenya, Ghana na wengine wengi alisema, akiwa Afrika Kusini atakaa kwa wiki moja kwa ajili ya kufanya mahojiano na wasanii wakubwa barani Afrika na kuripoti taarifa mbalimbali za kipekee kuhusu tuzo hizo kabla, wakati na baada ya tuzo.

lil-ommy-1

“Tunashukuru kwa nchi yetu kuwa na wasanii wengi zaidi kwenye tuzo hizi ambao wapo kwenye vipingele mbalimbali kama Yamoto Band, Navy Kenzo, Raymond, Vanessa Mdee na Diamond Platnumz hivyo kura zetu ndizo zitatoa majibu kesho.

“Nitakuwa nikiwajuza kila kinachotokea, hatua kwa hatua kabla na baada ya tuzo hizi. Kikubwa mnaweza kunifuatilia kupitia redio Times FM, mitandao ya kijamii kama Twitter, Instagram, Facebook, Periscope kwa jina la @LilOmmy pamoja na YouTube channel jina la LilOmmytv,” alisema Ommy.

The Playlist ni kipindi ambacho kinakaribisha mastaa ndani ya studio za 100.5 Times FM kila Jumamosi kuanzia Saa 6 hadi Saa 8 mchana lengo likiwa kusikia aina gani ya muziki ambao watu maarufu wanapenda kusikiliza, kila wiki ni star mmoja anaenda kuchangua nyimbo 5 anazopenda zaidi na kueleza kwanini huku kukiwa na mahojiano yaliojaa maswali yote muhimu.

Comments are closed.