The House of Favourite Newspapers

Salva Kiir Akutana na Museveni Uganda

0

Kiir na Museveni (1) Kiir na Museveni (2) Kiir na Museveni (4) Kiir na Museveni (5) Kiir na Museveni (6)

Na Leonard Msigwa/GPL

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ameitwa na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni kwenye Ikulu ya nchi hiyo na kufanya mazungumzo naye.

Ziara hiyo ya ghafla imekuja siku chache baada ya kutokea kwa mapigano makali kwenye mji wa Juba ambao ndiyo makao makuu ya nchi ya Sudan Kusini.

Mapigano hayo yalivihusisha vikosi vitiifu kwa Rais Kiir dhidi ya vile vinavyomuunga mkono Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Riek Machar ambaye mpaka sasa hajulikani wapi alipo tangu kuzuka kwa mapigano hayo.

Lengo la ziara hiyo ya ghafla ni kujaribu kutatua mgogoro baina ya Rais Kiiir dhidi ya makamu wake na baada ya mazungumzo hayo Rais Kiir amerejea nchini kwake.

Leave A Reply