The House of Favourite Newspapers

Wananchi: Mwanza Si Salama!

0

picha ya mwenyekiti enzi za uhai wake

Marehemu Nyenzi.

Na Johnson James, UWAZI

MWANZA: Kufuatia kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bubale, Kata ya Buhongwa,  Alphonce Mussa Nyenzi hivi karibuni, wananchi wa jiji hilo wameeleza wasiwasi wao wakidai sasa Mwanza si salama tena, Uwazi linakuhabarisha.

IMG_0024Mke wa marehemu nakilia kwa uchungu.

Maisha ya kiongozi huyo yalikatishwa baada ya kupigwa risasi na mtu asiyejulikana wakati akizungumza na wanandoa wawili njiani walioomba kusuluhishwa.

IMG_0057

Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili, kwa kuomba hifadhi ya majina yao kwa ajili ya usalama, wamesema wanapata hofu, hasa baada ya kubaini kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la mauaji ambayo yanawatisha, kwani wanaouawa ni viongozi na wananchi.

BODABODA WAKIUBEBA MWILI

Wakazi wa eneo la Bubale walisema tayari viongozi wawili wa mtaa huo, ambao wao wanawaona ni wazuri kwa sababu ya kusimamia sheria, wameuawa kwani kabla ya marehemu Alphonce, mtangulizi wake, Julius Kasabuku naye aliuawa.

IMG_0051

Wawakilishi wa wenyeviti wa mitaa katika Wilaya ya Nyamagana wameliambia gazeti hili kuwa hali ya sasa jijini Mwanza inatishia amani, hivyo kuanzia msiba huo uliotokea, wataanza kufanya sensa ili watu wafahamike katika mitaa yao, lakini pia wakaiomba serikali kuboresha ulinzi wao, kwani hivi sasa wanatamani kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na kuuawa.

_MG_0104

Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu.

Jumla ya watu 12 wameuawa mkoani Mwanza Mei mwaka huu, saba kati yao wilayani Sengerema ambao ni wa familia moja, huku Ilemela na Nyamagana zikishuhudia mauaji mengine ya watu wanne katika Msikiti wa Rahmani Mei 19, mwaka huu, hali iliyomfanya Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula kuona hali si salama na kushangaa kuona hakuna tamko linalotolewa na serikali katika kudhibiti hali hiyo.

WANACHAMA WA CCM WAKIUBEBA MWILI…Wakielekea kuzika.

“Nashangaa kuona wizara ya mambo ya ndani imekaa kimya kuhusu mauaji haya na mimi niwaahidi wananchi kuwa nitakapofika bungeni, mwongozi wangu wa kwanza kwa spika utakuwa ni kuhoji kwa nini halijatolewa tamko kuhusu suala hili,“ alisema Mabula.

IMG_0048Katika tukio la msiba wa Alphonce Mussa, wakati mwili wa marehemu ulipowasili ukitokea Hospitali ya Sekeu Toure ulikokuwa umehifadhiwa, mzozo ulitokea baina ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vijana wanaoendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, ambao walikuwa wakigombea kuupokea mwili huo na kuuingiza ndani ya nyumba yake.

Lakini baadaye wakakubaliana kuwa wanachama wenzake hao wauingize mwili huo ndani na vijana wa bodaboda watautoa tayari kuelekea makaburini. Ilipofika wakati wa kuutoa nje, vijana hao waliutoa nje, waliuzunguka na kufanya ibada fupi kabla ya wenyewe kuondoka eneo hilo.

baadhi ya wenteviti wa mitaa katika wilaya ya NyamaganaGetruda Alphonce, ambaye ni mke wa marehemu, aliiomba serikali kuwasaka wauaji wa mumewe na kuwakamata, ili sheria ichukue mkondo wake.

“Ninamshukuru Mungu ninaendelea vizuri, kwani mara nilipopewa taarifa hizi presha yangu ilipanda sana, sitamuona tena mume wangu,” alisema mke huyo huku akitokwa machozi.

Marehemu aliyeacha watoto 15, tisa kati yao wakiwa wa kike, alizikwa wiki iliyopita Kwimba alikozaliwa.

Leave A Reply