The House of Favourite Newspapers

Wasomaji Kigamboni Dar walichangamkia Ijumaa muonekano mpya!

0

1.Msomaji wa gazeti la Ijumaa,Pius Tamba (kushoto) akilinunua kwa muuzaji wa magazeti ya Global, Mwamvita Rashid.

2Msomaji wa Ijumaa Steven Paul (kulia) akilinunua gazeti kwa muuzaji.

3Msomaji wa gazeti la Ijumaa, Legan Mushi, akinunua gazeti kwa Mwamvita Rashid.

4Juma Mabina (kushoto) mkazi wa Kigamboni-Feri akinunua gazeti la Ijumaa kwa muuzaji.

5Anitha Deus mkazi wa Kibada Kigamboni (kushoto) akilinunua  Ijumaa kwa bei ya shilingi 1,000.

6.Wadau wa gazeti la Ijumaa wa eneo la Kigamboni-Feri wakilisoma gazeti hilo baada ya kulinunua.

7Wadau wa gazeti la Ijumaa wakiongozwa na mdau mkubwa wa gazeti hilo aliyejitambulisha kwa jina la Big Trans (wa kwanza kulia) wakipozi na muuzaji wa magazeti Mwamvita Rashid.

WASOMAJI mbalimbali wa Kigamboni Jijini Dar wamezidi kulifurahia gazeti la Ijumaa lenye muonekano mpya linalotoka mtaani kila siku ya Ijumaa.

Kamera yetu leo Ijumaa iliwafikia wakazi wa  Kigamboni, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo iliwashuhudia wasomaji mbalimbali wakijitokeza kwa wingi kwenye gari la matangazo la gazeti hilo  na kulinunua.

Akizungumza na wakazi eneo la Kibada, Kigamboni, Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers inayozalisha gazeti hilo pamoja na Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani na Championi, Yohana Mkanda, alisema anawaomba wasomaji wa magazeti hayo ya Global kuendela kulinunua Ijumaa kwa bei ya Sh.1,000 kwani limesheheni habari nyingi za burudani, hadithi, machombezo na mikasa.

“Magazeti yote ya Global yanauzwa kwa shilingi 500 isipokuwa Ijumaa pekee lenye muonekano mpya ndilo linauzwa shilingi 1,000. Niwasihi wasomaji wetu waendelee kununua magazeti yetu ili wazidi kuhabarika, kuelimika na kuburudika,” alisema Mkanda.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply