The House of Favourite Newspapers

Tinampay Amtisha Pialali, Naye Aapa Kumbomoa kwa KO – Video

0
Bondia Arnel Tinampay kutoka Ufilipino akitamba mbele ya kamera za Global TV Online na +255 Global Radio walipofika katika ofisi za Global Group, Sinza Mori jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya utambulisho wa pambano lake na bondia Idd Pialali watakalocheza Jumamosi, Novemba 28, 2020.

 

ARNEL Tinampay bondia Mfilipino aliyeko nchini sasa amesema atamtwanga Pialali mapema kwa sababu ameshamsoma anacheza kama bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo, hivyo kwake yeye kazi itakuwa nyepesi tu kumtwanga mpinzani wake huyo Mtanzania mapema.

Bondia Idd Pialali wa Tanzania akitamba mbele ya kamera za Global TV Online na +255 Global Radio walipofika katika ofisi za Global Group, Sinza Mori jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya utambulisho wa pambano lake na bondia Arnel Tinampay wa Ufilipino watakalocheza Jumamosi, Novemba 28, 2020.

 

Naye Pialali anasema yeye na Mwakinyo ni mabondia tofauti na hawezi kufananishwa na bondia yeyote hapa nchini kwani ana uzoefu mkubwa na mashindano mengi makubwa ya kimataifa, uwezo wake na mbinu za mwalimu wake, hivyo Mfillipino huyo asijidanganye, atamtwanga kwa KO kwani hatorudi tena Tanzania.

Bondia wa Tanzania, Idd Pialali (kushoto) akiongozana na bondia mwenzake, Arnel Tinampay kutoka Ufilipino (kulia) wakiwasili katika ofisi za Global Group, Sinza Mori jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya utambulisho wa pambano lao watakalocheza Jumamosi, Novemba 28, 2020.

 

Shughuli itakuwa pevu pale Next door Masaki jijini Dar es Salaam ambako tayari tikezi za pambano  zinauzwa kwa kiingilio cha sh 20,000 mzunguko, Sh 50,000 kawaida na Sh 100,000 kwa VIP.

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers na mchambuzi maarufu wa masuala ya michezo hapa nchini, Saleh Ally ‘Jembe’ (katikati) akiwatambulisha; Bondia Arnel Tinampay kutoka Ufilipino (kushoto) na Bondia wa Tanzania, Idd Pialali (kulia) wakati mabondia hao walipowasili katika ofisi za Global Group, Sinza Mori jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya utambulisho wa pambano lao watakalocheza Jumamosi, Novemba 28, 2020.

Tiketi hizo zinapatikana kupitia Nilipe App,Selcom,Vunja Bei Store na Vunja Bei Toto Sinza, Shishi Food Kinondoni, Cake City Njiapanda ya SalaSala, Kaites Lounge Tabata na Dick Sound Magomeni.

Kutoka kushoto ni mabondia wa Ufilipino, Eduardo Mancito na Arnel Tinampay, katikati ni Mwandishi wa Magazeti ya Championi na Spoti Xtra, Ibrahim Mussa pamoja na mabondia wa Tanzania, Salim Mtango na Idd Pialali walipowasili katika ofisi za Global Group, Sinza Mori jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya utambulisho wa pambano lao watakalocheza Jumamosi, Novemba 28, 2020.

Pambano hilo limedhaminiwa na Gazeti jipya na bora la michezo nchini…. #SpotiXtraJumanne
Pamoja na: @255globalradio

 

Leave A Reply