The House of Favourite Newspapers

Said Fella, ‘Upendo Ni Mimi’ Wachangia Damu Temeke

299d9708-bd8e-4fca-88ae-8f32a29ec2d6 8902b5b8-6cbf-45f5-8670-a7685187bc93 30045101-6fed-4f08-8847-2822b29b5dfa cfcb0caa-1c8c-4aca-a6c2-debd43d2f2e6 d9f73364-80e9-4865-8515-8d53c576a5c8 e5d2144f-4b9c-40c0-ad74-af3cc86117d3 4be2e6a9-2539-45fe-ac6f-846c77a322fe 89a3edec-fe46-4fe2-8fe5-ed43b6efd231Wanachama wa Taasisi ya Upendo ni Mimi wakichangia damu katika Hospitali ya Temeke.

NA GABRIEL NG’OSHA/GPL

Said Fella, ‘Upendo Ni Mimi’ Wachangia Damu Temeke

DIWANI wa Kata ya Mbagala Kilungule, Said Fella, na Taasisi ya Upendo ni Mimi leo wamejitokeza kuchangia damu katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusaidia wahitaji wa huduma hiyo.

Taasisi ya Upendo ni Mimi ina jumla ya wanachama hai 20, ikiwa na lengo la kutoa misaada wa makundi maalumu wakiwemo watoto yatima na walemavu, kutoa elimu ya kuzuia na kujijkinga na matumizi ya dawa za kulevya, ndoa za utotoni na kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi.

Sisi kama Upendo ni Mimi tumejipanga kurudisha tumaini na faraja kwa makundi maalumu kwa sababu wamesahaulika na ndiyo maana leo tumeamua kujitolea kuchangia damu katika hospitali yetu. Tunamshukuru diwani Fella kwa ushirikiano wake,” alisema Meneja Mradi wa Upendo ni Mimi, Hamza Issa.

Jumla ya wachangiaji 60 walijitokeza kuchangia damu akiwemo msanii Kayumba Juma, Salam TMK, Omarly Clyton na wengine wengi.

Comments are closed.