The House of Favourite Newspapers

Tuzo za Flora Lauwo Zazua Balaa

Flora Show (kushoto) akiwa na baadhi ya wabunge

MWANZA: Mtangazaji wa Kipindi cha Flora Show ambaye ni mkurugenzi wa taasisi yake ya Nitetee Foundation Tanzania, Flora Lauwo amezua balaa kufuatia tuzo alizozitoa Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, mwaka huu, Mwanza ambapo wengi wamesema zilijaa sintofahamu. Kwa mujibu wa chanzo chetu, Flora alitoa tuzo hizo kupitia taasisi hiyo kwa kuacha wengine waliotakiwa kupewa kwani kwa uchambuzi wa kawaida, hakufanya usawa.

Frola (kulia) akiwa na mmoja wa walezi wa kituo cha watoto yatima

“Unajua ilivyo ni kwamba, zile tuzo za Nitetee Foundation zilikuwa nzuri tu na hata watoa tuzo pia ni wazuri, ila sasa kuna walioachwa ambao kusema kweli hawakutakiwa kuachwa.

“Unatoaje tuzo kwa benki kongwe nchini halafu unaiacha benki nyingine kongwe pia ambayo ina jina kubwa na wateja wengi. “Unatoaje tuzo kwa msanii ambaye hajafanya kazi yoyote ya kijamii ambayo ilipendwa au ilisaidia jamii? Ukweli kama Flora ataandaa na kutoa tuzo kama hizo mwakani, akaacha wengine wenye sifa, ataharibu.

Tuzo (Mfano)

“Kwanza hata siku ile ukumbini mwenyewe aliona, maneno yalikuwa ni mengi sana. Watu walikuwa wakisema maneno ya chini kwa chini kwamba kuna kaupendeleo ka waziwazi, kwamba wengine waliachwa lakini walistahili kupewa, ingawa waliopewa pia walikubalika,”kilisema chanzo hicho.

Ili kupata uwiano wa malalamiko hayo, juzi Wikienda lilizungumza na Flora ambaye  alikiri kusikia malalamiko hayo na kusema: “Yaani kusema ule ukweli hakukuwa na upendeleo wowote ule. Nimesikia watu wakinisakama kwamba kuna niliowaacha waliostahili kupewa, kama akina nani sasa?

“Ninavyojua siku zote, unapofanya kitu chochote katika jamii, lazima watatokea watu wa kwenda kinyume, hata kama ni kitu cha kupigiwa kura na wengi.

“Ila maoni yao ni mazuri, mara nyingine tutaangalia namna ya kumfurahisha kila mtu.”

Baadhi ya watu maarufu na taasisi walionyakua tuzo hizo ni Vicky Kamata (Sanaa na Utamaduni), Getrude Mongela (Uongozi), Anna Tibaijuka (Uongozi), Angelina Mabula (Msimamo), Mama Maria Nyerere (Heshima), CRDB (Tuzo Maalum), Vodacom (Tuzo Maalum) na wengine wengi.

 

Comments are closed.