The House of Favourite Newspapers

Baghdad Kula Sahani Moja na Serikali

Baghdad akiwa na wacheza shoo wake.

Na ALLY KATALAMBULA| GAZETI UWAZI| SHOWBIZ

RAPA ambaye ni miongoni mwa wasanii wanaounda Kundi la Mexcana la Vavela, Baghdad anayetamba kwa sasa na Wimbo wa Usinipangie, amesema kuwa hata ikiwa kupitia nyimbo zake atakazokuwa anatoa hasa za kuikosoa serikali zitamfanya akamatwe na polisi kwa namna yoyote ile lakini hatakoma kutoa nyimbo hizo maana hawezi kupangiwa kufanya kazi yake.

Akistorisha na Uwazi Showbiz, Baghdad aliongeza kuwa msanii hasa anayefanya Muziki wa Hip Hop ambaye ataogopa mikimiki ya serikali pale anapofanya kazi yake atakuwa si imara na hafahamu umuhimu wa kazi yake na nini anatakiwa kufanya kama msanii kwenye kazi yake hiyo.

“Mimi nitakula sahani moja na serikali pale inapokosea na wala siwezi kuogopa wala kufungwa mdomo na yeyote yule, ninafahamu ninachokifanya na kipi kinatakiwa kiwafikie mashabiki wangu tena kwa wakati ambao ninautaka mimi,” alisema rapa huyo.

 

Comments are closed.