The House of Favourite Newspapers

Pluijm ataka kipa mpya Singida United

0
Kocha Mkuu wa Singida United ya Singida, Mholanzi, Hans van Der Pluijm.

KOCHA Mkuu wa Singida United ya Singida, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, raia wa Uholanzi, ameutaka uongozi wa timu hiyo kuipata saini ya kipa yeyote mkongwe kwa ajili ya kukichezea kikosi hicho msimu ujao.

Mratibu wa Singida United, Festo Sanga ameliambia Championi Jumatatu kuwa Pluijm amependekeza kusajiliwa kwa kipa mpya atakayekuja kufanya kazi na makipa waliopo kwa ajili ya kuiboresha safu yake ya ulinzi.

Leave A Reply