The House of Favourite Newspapers

SHABIKI AVAMIA UWANJA KUMKUMBATIA WAYNE ROONEY!

0
Kikosi cha timu ya Everton kilichoanza dhidi ya Gor Mahia katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Julai 13.
Kikosi cha Gor Mahia kilichoanza dhidi ya Everton.
Mchezaji wa Gor Mahia, Mussa Mohammed (kulia) akimtati Wayne Rooney.
Mashabiki mbalimbali wakiendelea kunagalia mechi hiyo.
Wakiwania mpira wakati wa mchezo.
Shabiki akiwa amemkumbatia Mshambuliaji wa Everton Wayne Rooney (katikati).
…Akitolewa nje ya uwanja na polisi.

Shabiki mmoja ameshindwa kujizuia baada ya kutoka jukwaani na kuingia hadi uwanjani kwenda kumkumbatiamshambuliaji wa Everton Wayne Rooney wakati wa mechi ya kirafiki kati ya Gor Mahia dhidi ya Everton.

Rooney alikuwa amezungukwa na mabaunsa zaidi ya watatu nje akiwa nje ya uwanja ili kupunguza usumbufu wa watu waliokuwa wakitaka kupiga nae picha ‘selfie’.

Jamaa huyo ambae alikuwa amevaa jezi ya Manchester United hakufahamika jina lake mara moja alikimbia kutoka jukwaani na kukatiza uwanjani hadi kwa Roone na kumkumbatia.

Kwenye mechi hiyo, Rooney amefunga goli lake la kwanza tangu arejee Everton akitokea Manchester United sehemu aliyopata umaarufu mkubwa kutokana na mafanikio aliyoyapata.

Mechi hiyo imemalizika kwa Everton kupata ushindi wa magoli 2-1. Everton walitangulia kufunga goli la kwanza ambalo lilipachikwa na Rooney kisha Medie Kagere akaisawazishia Gor Mahia kabla ya Dowell kufunga bao la pili kwa Everton.

PICHA: RICHARD BUKOS NA MUSA MATEJA, GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply