The House of Favourite Newspapers

Stars Kuifuata Rwanda Leo

0
Wachezaji wa timu ya Taifa Stars wakiwania mpitra na mchezaji wa Rwanda aliye katikati.

KIKOSI cha Taifa Stars kinatarajia kuondoka nchini leo Jumatano kuelekea Rwanda kwa ajili ya kuikabili timu ya taifa hilo, Amavubi.

 

Taifa Stars itatokea Mwanza na kuunganisha safari ambapo ikitua Dar, itapanda ndege ya Shirika la Rwanda Air kuelekea huko.

 

Taifa Stars inatarajia kurudiana na Amavubi Jumamosi ijayo ya Julai 22, badala ya Jumapili ya Julai 23, mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali kufuatia wenyeji wao hao kuwataarifu Caf kuwa mchezo huo uchezwe Jumamosi.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Afred Lucas, alisema wamepata taarifa kutoka Caf juu ya mabadiliko ya mchezo huo ambapo mwalimu amelazimika kubadili ratiba ya siku moja na kikosi kuondoka nchini leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.

 

Wakati huohuo, Kamati ya Uchaguzi wa Chama cha Wataalamu wa Tiba za Michezo (Chawatimita- Tasma) imetangaza majina 12 ya wagombea mbalimbali katika chama hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 5 baada ya zoezi la uchukuaji fomu kukamilika Julai 17.

Stori: Khadija Mngwai | Championi Jumatano

Leave A Reply