The House of Favourite Newspapers

Beyonce Aajiri ‘Mabeki Tatu’ Sita

0
Mwanamuziki wa R&B, Beyoncé Giselle Knowles.

AJIRA! Wasich-ana sita wamepata ajira kwenye familia ya mastaa Beyonce na mumewe Jay Z ambao ni wasanii wakubwa duniani, kwa ajili ya kuwalea watoto wao mapacha.

Juni mwaka huu, Beyonce ambaye anaimba Muziki wa R&B pamoja na Jay Z anayekamua Hip Hop, walipata watoto mapacha waliowapa majina ya Rumi na Sir Carter. Usisahau kuwa kuna wadada wengine wawili ambao wanamlea mtoto wao wa kwanza, Blue Ivy.

Wafanyakazi hao watakuwa wakilipwa dola 100,000 (Sh milioni 221.4) kila mmoja kwa mwaka huku wakiwekewa zamu tofauti za kulala nao na kuwalea mapacha hao kwa muda wote huko Los Angeles ambako ndiyo kuna makazi ya wasanii hao.

Kwa maana hiyo, ukipiga hesabu utaona nyumbani kwa Beyonce na Jay Z tayari kuna wasaidizi nane yaani ukichanganya wale sita na wawili wa Blue Ivy ndiyo unapata idadi hiyo ya ‘mabeki tatu’.

Ziggy: Sitaki Kuitwa Msanii Wa Bongo Movie

Leave A Reply