The House of Favourite Newspapers

16 Bora Afcon 2019… Moto utawaka balaa

HATUA ya makundi ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) inayofanyika nchini Misri, ilimalizika Jumanne ya wiki hii kwa kuchezwa mechi za Kundi E na F.

Mechi hizo zilitoa taswira ya timu 16 ambazo sasa zitapambana kwenye Hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya 32 sasa.

 

Timu zilizotinga hatua hiyo ni Misri, Uganda na DR Congo kutoka Kundi A. Kundi B zimepita Madagascar, Nigeria na Guinea, huku Kundi C Algeria na Senegal zikivuka.

Kundi D timu zilizopita ni Morocco, Ivory Coast na Afrika Kusini. Kundi E ni Mali na Tunisia, wakati Kundi F ambalo ni la mwisho, Ghana, Cameroon na Benin nazo zimepita.

 

Tayari ratiba ya mechi za hatua hiyo imeshajulikana ambapo hapo sasa moto utawaka zaidi tofauti na tulivyoshuhudia katika hatua ya makundi.

Katika makundi hayo, timu mbili za juu ndizo zimesonga hatua ya 16 Bora moja kwa moja, huku nne zikipenya kwa sheria ya ‘best looser’ ambazo ni Afrika Kusini, Benin, DR Congo na Guinea.

 

Ratiba inaonyesha kuwa, leo Ijumaa kutakuwa na mechi mbili ambapo Morocco iliyoshinda mechi zote tatu za hatua ya makundi ikiwa Kundi D, itapambana na Benin iliyovuka kama ‘best looser’ kutoka Kundi F.

Pia Uganda ambayo imeshika nafasi ya pili Kundi A, itakuwa na kibarua cha kupambana na Senegal ambayo nayo imemaliza nafasi ya pili Kundi C.

 

Hii itakuwa mechi ya tatu kwa Senegal kucheza dhidi ya timu kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya hatua ya makundi kuzifunga Tanzania mabao 2-0 na Kenya kuchapwa 3-0.

Mechi zingine hatua hiyo ni Nigeria vs Cameroon, Misri vs Afrika Kusini, Madagascar vs DR Congo, Algeria vs Guinea, Mali vs Ivory Coast na Ghana vs Tunisia.

CAIRO, Misri

JPM: Kenyatta ‘Aniombe Radhi’, Hatukukubaliana Watufunge Mabao 3-2- Video

Comments are closed.