The House of Favourite Newspapers

JINI KABULA AENDELEA KUWAGUSA WENGI

0
Mwigizaji Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.

MUDA mfupi baada televisheni ya mtandaoni inayoongoza kwa kutazamwa na wengi zaidi ya Global TV Online kujitokeza kuendesha kampeni maalum ya kumchangia fedha za kusaidia matibabu na huduma kwa mwigizaji Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ijulikanayo kwa Jina la Support Treatment For Jini Kabula, watu wengi wameendelea kuguswa na suala hilo hivyo kuanza kujitolea kwa moyo kwa kadiri walivyojaliwa.

 

Kwa nyakati tofauti, baadhi ya watu hao walizungumza na mwandishi wetu kupitia simu ya mkononi ambapo walieleza hisia zao namna ambavyo wameguswa na tatizo la Kabula baada ya kutazama mahojiano yake kupitia Global TV Online.

 

“Binafsi nimeguswa sana na tatizo la Kabula hivyo kwa chochote nitakachojaliwa nitajitolea kwa ajili ya kusaidia, ninaamini na wengine wataguswa kama mimi, maana najua Watanzania tuna moyo wa upendo na mshikamano kwenye matatizo,” alisema mmoja wa wadau waliozungumza na mwandishi wetu.

 

Kwa mujibu wa ndugu wa Kabula, kwa mtu yeyote anayeguswa na tatizo la ndugu yao na yupo tayari kujitolea kumsaidia kwa chochote, basi atume mchango wake kupitia simu ya mkononi kwa namba: 0712 56 53 69 ambapo jina litasomeka Daynes Jolwa ambaye ni dada wa damu wa Jini Kabula.

 

KUTOA NI MOYO SI UTAJIRI. KWA CHOCHOTE KIDOGO, TUJITOLEENI KUMSAIDIA MSANII HUYU KWANI MATATIZO HUZUNGUKA, LEO KWAKE, KESHO UNAWEZA KUWA WEWE AU NDUGU YAKO. ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI SANA-GLOBAL TV ONLINE

Esha Buheti: Jini Kabula Kweli Anaumwa, Tumsaidieni!

Leave A Reply