The House of Favourite Newspapers

Kapombe: Yanga SC Tunawalaza Mapema

0

 

Beki wa Simba, Shomary Kapombe.

BEKI wa Simba, Shomary Kapombe, amesema kwa sasa anaendelea vizuri na majeraha ya nyonga yaliyokuwa yakimsumbua baada ya kupona na yupo tayari kuanza mapambano na kwamba leo Simba itashinda tu kwani wachezaji wenzake waliopo wana uwezo mkubwa.

Kapombe ambaye mara kwa mara amekuwa akisumbuliwa na tatizo hilo, hivi karibuni alijitonesha wakati akiitumikia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilipocheza dhidi ya Rwanda kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki Michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan).

Akizungumza na Championi Jumatano, Kapombe amesema mchezo wa leo mbele ya watani zao, Yanga ana imani kubwa na kikosi kilichopo hivyo ana matarajio makubwa na ushindi.

“Kwa sasa naendelea vizuri kwani yale majeraha yangu yamepona na sisikii maumivu, muda wowote naweza kuungana na wenzangu kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao, sifurahii kukaa nje, nimekuwa nikipambana kuhakikisha napona haraka na kurejea uwanjani kuipambania timu yangu, kitu cha faraja ni kwamba kwa sasa naweza kufanya hivyo kutokana na kupona.

“Kuhusu mchezo wa leo wa Ngao ya Jamii nina imani na wachezaji wenzangu watatuwakilisha kwa ushindi hivyo, sina hofu kwani timu yangu ina uwezo wa kushinda bila mimi,” alisema Kapombe.

Stori: Musa Mateja, Championi Jumatano

Leave A Reply