The House of Favourite Newspapers

Matola: Yanga Hawana Plani B

0
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akimtoka beki wa Lipuli.

BAADA ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga, Kocha wa Lipuli FC, Selemani Matola amewazungumzia wapinzani wao hao kwa kusema kuwa hata kama mchezo wao ungekuwa wa dakika 200 kamwe wasingefungwa na Yanga.

Timu hizo zilikutana katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar, Jumamosi iliyopita ambapo Lipuli iliibana vizuri Yanga na kuwafanya mabingwa hao watetezi kukosa nafasi ya kufanya vizuri katika vipindi vyote viwili. Matola, kiungo na kocha wa zamani wa Simba ameuzungumzia mchezo huo kwa kusema kuwa Yanga hawakuwa na mbinu mbadala, badala yake plani yao ni ileile ambayo waliitumia pia katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambapo wao Yanga walipoteza.

Mchezaji wa Lipuli (kushoto) akimtati Donald Ngoma.

“Yaani nilianza kuwasoma kuanzia katika mchezo wao na Simba, niliwasoma vizuri na nikawa nimeshawajua kila kitu chao, ajabu nilipokutana nao walitumia mbinu zilezile na walicheza vilevile kama walivyocheza na Simba ndiyo maana tukawabana.

“Ilinishangaza kidogo kuona kipindi cha kwanza wanacheza kama walivyocheza na Simba, hata bao lao wenyewe si umeona la kubahatisha tu, nilitegemea wangebadilika kipindi cha pili baada ya kuona tumewabana kipindi cha kwanza lakini waliingia wakiwa na mbinu zilezile.

“Hivyo, hata kama tungeendelea kucheza nao kwa dakika 200 bado matokeo yangekuwa yaleyale au sisi kuwafunga wao lakini wao wasingeweza kutufunga,” alisema Matola. Alipoulizwa anahisi sababu ipi ilichangia Yanga kutobadili mbinu muda wote wa mchezo wao licha ya kubanwa, Matola alisema: “Hilo nafikiri ni suala lao wao na benchi lao la ufundi, wao ndiyo wanatakiwa kujibu. Hawakuwa na plani B.”

Na John Joseph, Dar es Salaam

William Ngeleja: Seduce Me ya Alikiba Sio Level ya Bongo

Makamba, Shaka, Shigongo, Sarungi, Marsha Kukutana Kwenye Meza ya Wazalendo


Leave A Reply