The House of Favourite Newspapers

SMG ampa Lwandamina mbinu kuiboresha Yanga (Video)

0

WINGA wa zamani wa Yanga, Said Maulid ‘SMG’ amemwambia kocha mkuu wa timu hiyo Mzambia, George Lwandamina, kama anataka timu hiyo ipate matokeo mazuri kwenye mechi za Ligi Kuu Bara, basi abadili mfumo na aina ya uchezaji anayoitumia.

 

Yanga hadi sasa imecheza michezo mitano ya ligi kuu na kufanikiwa kupata ushindi kwenye mechi mbili pekee dhidi Njombe Mji na Ndanda.

 

Timu hiyo ilipata sare dhidi ya Lipuli FC, Majimaji na Ndanda FC na kufanikiwa kupata pointi tisa.
Akizungumza na Championi Global TV Online ya Spoti Hausi, SMG alisema asili ya soka la Yanga ni la mipira mirefu (counter attack) huku wakiwatumia mawinga katika kutengeneza mabao na siyo kujaza viungo wengi na kupiga pasi nyingi.

 

SMG alisema, mfumo huo wa kujaza viungo wengi badala ya kuwatumia mawinga waliokuwepo akina Geofrey Mwashiuya, Mussa Said (aliyepandishwa kwenye kikosi cha wakubwa) na Burhani Akilimali ndiyo sababu ya Yanga kupata matokeo mabaya.

 

Aliongeza kuwa mfumo huo unawatesa washambuliaji akina Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu wanaofanyakazi mara mbili ya kufuata mipira chini kwa viungo ili waende kushambulia kwenye goli la wapinzani.
“Nikwambie tu, Yanga asili yake ni soka la counter attack na siyo soka la pasi, nikuhakikishie kama Yanga wakiendelea na mfumo huo wa uchezaji, basi timu hiyo itaendelea kupata matokeo mabaya katika mechi zake za ligi kuu.

 

“Kwa sababu Yanga inatumia mashambulizi yake kupitia pembeni huku ikiwatumia mawinga wazuri na mabeki wa pembeni kwa ajili ya kupiga krosi na kufunga mabao, utaona kwenye msimu huu katika mechi hizi za ligi kuu huvioni vitu hivyo vikifanyika.

 

“Na hiyo imetokana na kocha kujaza viungo wengi katika timu huku akitaka mabao yatengenezwe kupitia katikati, hiyo siyo asili ya Yanga. Niseme Yanga mabao yao wanatengeneza kupitia pembeni.

 

“Yanga wanapata tabu katika timu msimu huu baada ya Msuva (Simon) kuondoka kwani hawana mbadala mwingine anayeweza kucheza kama yeye. Kama unakumbuka, aliondoka winga Akida (Makunda) nikaja mimi na nilipondoka mimi akaja Ngassa (Mrisho) ambaye naye aliondoka akaja Msuva. Hivyo basi, Yanga inatakiwa imtengeneze winga mwingine wa kulia mwenye kasi ambaye yupo ninaamini na kikubwa ni kumuamini,” alisema SMG ambaye ni hivi karibuni alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Soka la Vijana wa Yanga.

Leave A Reply