The House of Favourite Newspapers

Kimenuka Upya! Soo La Zari, Mobeto Latinga Polisi!

0
Zarinah Hassan Tiale ‘Zari The Boss Lady’.

DAR ES SALAAM: Hatimaye lile soo baab’kubwa la bifu kati ya mwanamitindo na video ‘vixen’ matata wa Bongo, Hamisa Hassan Mobeto na mwanamama mjasiriamali wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan Tiale ‘Zari The Boss Lady’, limetinga polisi, Risasi Mchanganyiko limetonywa.

KWANI ILIKUWAJE
Sakata hilo linadaiwa kuchukua sura mpya baada ya Hamisa kuundiwa zengwe kwenye mitandao ya kijamii na watu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wa makosa ya kimtandao.

Zengwe hilo ambalo linadaiwa kufanywa na watu wasiojulikana kwa kujifanya ni wanasheria wa Kampuni ya Danube inayohusika na uuzaji wa fenicha, linaeleza kuwa, mwishoni mwa wiki iliyopita, ilimuandikia Hamisa barua, eti ikimtaka afute posti kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

Video ‘vixen’ matata wa Bongo, Hamisa Hassan Mobeto.

Ilielezwa kuwa, posti hiyo aliyotakiwa kuifuta ni ile inayomuonesha Zari akizozana na mzazi mwenzake juu ya hereni za Hamisa ambazo zilidaiwa kukutwa na Zari nyumbani kwa mwanaume huyo, Madale, nje kidogo ya Jiji la Dar.

 

Katika ukurasa wake wa Instagram, Hamisa aliweka ‘clip’ na ‘kuitag’ kwenye ukurasa wa Kampuni ya Danube kisha kusindikizia maneno yaliyosemeka; “Its about time’ nifuate hereni zangu. I hope it’s still there!”
Ujumbe huo ulizua zogo katika mitandao ya kijamii, lakini muda mfupi baadaye, zogo hilo lilihamia kwenye barua iliyosambaa, iliyodaiwa kuandikwa na kampuni moja ya mawakili (jina linahifadhiwa) ikimpa onyo kali Hamisa kuacha kutumia bidhaa zao kwa maslahi yake binafsi.

Kufuatia kasheshe hilo, Risasi Mchanganyiko liliutafuta uongozi wa Danube ili kupata ukweli juu ya utata wa barua hiyo ambapo mmoja wa maafisa wake alifunguka;

 

“Ninachoweza kusema ni kwamba sisi hatujui chochote kuhusu ujumbe kwa Hamisa, barua inayosemwa imetoka kwetu na zengwe lililoibuka huko mtandaoni.
“Vyote hivyo, ni vitu vipya kwenye macho na masikio yetu. Kiukweli hakuna chochote tunachohusika nacho,” alisema jamaa huyo.

 

Ofisa mwingine wa kampuni hiyo ambaye naye hakutaka jina lake kutajwa, alisema saini na jina la mwanasheria aliyesaini barua iliyopelekwa kwa Hamisa, siye anayetambuliwa na kampuni yao.

 

KAULI KUTOKA KWA MAMA MOBETO
Baada ya kusikia kauli hiyo, gazeti hili lilimtafuta Hamisa kupitia simu yake ya mkononi na alipopokea, baada ya kuulizwa kuhusu ishu hiyo, alimtaka mwandishi wetu kupiga baada ya muda kwani alikuwa na kitu anafanya, hata hivyo, alipopigiwa baadaye, simu yake haikupatikana.
Lakini mama yake mzazi, ambaye mara nyingi huongea kwa niaba ya mtoto wake, alisema watu wasifuate sana mambo ya mtandaoni kwa sababu mengi huwa siyo ya kweli.

 

MAKOSA YA KIMTANDAO HAWA HAPA
Kwa kutambua kuwa, katika sakata hilo kunaweza kuwa na harufu ya kosa la kimtandao, Risasi Mchanganyiko liliwatafuta watu wa kitengo cha Jeshi la Polisi kinachohusika na makosa ya kimtandao kupitia bosi wake aliyejitambulisha kwa jina moja la Joshua.

 

Katika mazungumzo yake, mkuu huyo wa kitengo alisema bado dawati lao halijapata malalamiko hayo ingawa yeye binafsi amekuwa akiliona tukio hilo mitandaoni.

 

“Sheria za makosa ya kimtandao ziko wazi, anatakiwa aidha, Hamisa au Kampuni ya Danube ilete malalamiko yao mezani kwetu, sisi tutayashughulikia, ingawa ninaamini kabisa faili hilo tayari litakuwa katika moja ya vituo vya chini likishughulikiwa maana uhalifu huo hata mimi nimeuona,” alisema Kamanda Joshua.

Waandishi: Gladness Mallya, Imelda Mtema na Ally Katalambula

Leave A Reply