The House of Favourite Newspapers

Yanga: TFF Wanatuvuruga

0
Wachezaji wa Yanga na Simba.

SIKU chache baada ya uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kusema kuwa Tanzania Bara itashiriki michuano ya Chalenji itakayofanyika nchini Kenya, uongozi wa Yanga umedai kuwa michuano hiyo itawavurugia mipango yao waliyojiwekea kwa ajili ya Ligi Kuu Bara msimu huu.

 

Michuano ya Chalenji ambayo hushirikisha timu za taifa za nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Ce­cafa), imepangwa kuanza Novemba 25 huko nchini Kenya.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alisema wao walikuwa wamejipanga kwa kuzingatia ratiba ya awali ya ligi kuu ambayo ilikuwa haionyeshi kama kutakuwepo na mashindano ya Cha­lenji.

“Ligi inaposimama kila wakati hakika inatu­vurugia mipango yetu ambayo tulikuwa tu­mejiwekea kwa ajili ya kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu.

 

“Kama walijua kabisa kuwa safari hii tuta­shiriki michuano ya Chalenji walipaswa kutu­julisha mapema katika ratiba ligi kuu kabla ya kuanza kwa ligi ili tuweze kupanga mikakati yetu tukijua kuwa itakapofika tarehe fulani ku­takuwa na hiki siyo kutukurupusha namna hii.

 

“Wanatuvurugia mipango yetu lakini pia wanatuongezea gharama za uendeshaji wa timu, kwa sababu katika muda huo ambao ligi itakuwa imesimama tutalazimika kuiweka timu kambini kwa muda mrefu kitu ambacho hakikuwa kwenye mipango yetu,” alisema Mk­wasa.

  Stori: Sweebert Lukonge na Martha Mboma

SPOTI HAUSI: Kipa Wa Simba Afunguka Kisa Cha Yanga Kufungwa Bao 5 na Simba

Leave A Reply