The House of Favourite Newspapers

Okwi, Niyonzima Waondolewa Simba

Emannuel Okwi.

KAIMU Kocha wa Simba, Masoud Djuma amewaondoa kikosini wachezaji Haruna Niyonzima na Emannuel Okwi kutokana na majeraha yao ya muda mrefu na kudai kuwa hawategemei katika timu yake kwani ana kikosi kipana.

 

Okwi na Niyonzima hawakushiriki katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kutokana na majeraha ya enka waliyoyapata katika mechi za Ligi Kuu Bara hivi karibuni.

Haruna Niyonzima.

Okwi raia wa Uganda ndiye kinara wa mabao katika ligi kuu akiwa na mabao nane hadi sasa huku akifuatiwa na Habib Haji wa Mbao FC mwenye mabao saba.

 

Hata hivyo, tayari Niyonzima raia wa Rwanda ameshaanza mazoezi mepesi ya kujiweka sawa.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Djuma alisema ; “Simba haina wachezaji wawili na siyo kutokuwepo kwa Niyonzima na Okwi ndiyo kulikosababisha kutolewa mapema Mapinduzi, timu ina wachezaji wengi wenye uwezo na hata uongozi unajua.”

 

“Sitaweza kuwatumia Niyonzima na Okwi hadi watakapokuwa tayari kucheza kwa kuwa fiti na kwa sasa bao hawapo fiti, wakiwa vizuri watacheza na kukisaidia kikosi.

 

“Simba ina wachezaji wengi wazuri, hivyo naamini waliokuwepo watafanya vizuri ndiyo maana uongozi ulisajili wachezaji wengi, hao watatusaudia katika mechi zetu,” alisema Djuma ambaye alikuwa kocha na mchezaji wa zamani wa Rayon Sports ya Rwanda.

 

Wakati Niyonzima akiichezea Simba kwa mara ya kwanza msimu huu akitokea Yanga alikomaliza mkataba, Okwi yeye anaichezea timu hiyo kwa mara ya tatu baada ya kusajiliwa mara mbili huko nyuma.

 

Baada ya kutolewa katika Kombe la Mapinduzi, Alhamisi ijayo Simba itacheza na Singida United mechi ya ligi kuu.

jijini Dar es Salaam.

ALICHOKISEMA NSAJIGWA BAADA YA KUWASILI SABABU YA CHIRWA KUKOSA PENALTI

Comments are closed.