The House of Favourite Newspapers

2-face awaomba Don Jazzy, D’banj waanzishe tena ushirikiano

0

Mwanamuziki maarufu wa Nigeria, 2-Face Idibia.

Lagos Nigeria

MWANAMUZIKI maarufu wa Nigeria, 2Face Idibia, ametoa wito kwa wanamuziki wawili nchini mwake, Don Jazzy na D’Banj kufikiria kuungana ili kutoa wimbo mmoja, kwani yeye anawaheshimu sana wawili hao kimuziki.

2Face Idibia aliyesema hayo kwenye onyesho la Fortyfied Concert lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kuadhimisha mwaka wa 40 wa kuzaliwa kwake akiwa jijini Lagos. Aliwaomba magwiji hao wa muziki kuungana na kutoa kibao kimoja kikali.

Wakati D’Banj alipanda jukwaani na kutumbuiza kwa wimbo wake wa ‘I’m Feeling’ ambao prodyuza wake ni Don Jazzy akishirikiana na 2Face, miaka kadhaa iliyopita, Don Jazzy, aliwashangaza mashabiki alipokataa kushiriki wimbo huo.

Don Jazzy anasemekana alikikataa kipaza sauti alichopewa na kutazama kwengine.
Mwaka 2012, Don Jazzy na D’Banj, waasisi wa kampuni ya muziki ya Mo’Hits, walitengana ambapo Don alianzisha kampuni ya Mavin Records, wakati D’Banj alianzisha kampuni ya DB Records.

JIUNGE NA GLOBAL BRAKING NEWS UPATE HABARI KEMKEM ZA UCHAGUZI MKUU

globalbreakingnews.JPG

Leave A Reply