KITUO cha Uwekezaji nchini (TIC) kimetakiwa kuwa kivutio kikubwa kwa wawekezaji kwa kufanya kazi kwa weledi na bidii kwa kuwa ndio kinatazamwa na matajiri hao.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (katikati) akikata utepe kuzindua kituo cha uwekezaji TIC.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage alipokuwa akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye kituo hicho wakati wa uzinduzi wa huduma mahala pamoja katika kituo hicho.
Mwijage (kushoto) akiangalia ndani ya ofisi hiyo sehemu ya wafanyakazi wa kituo hicho wanapofanyia kazi zao.
Mwijage akifafanua wakati wa uzinduzi wa huduma za mahala pamoja pa kazi, alisema kituo hicho kinatakiwa kutoa huduma bora ili taarifa ziweze kuwa za wazi kwenye taasisi za umma na kuongezeka kwa pato serikalini.
Mwijage (kushoto) akionyesha hisia zake kwa wafanyakazi hao wa TIC wakati akizungumza nao jambo.
“Nyie wafanyakazi wa kituo cha uwekezaji ni vizuri mkafanya kazi kwa kujituma na uwazi ili kuwezesha wawekezaji kutopata tabu wanapokuja kutafuta fursa za uwekezaji na hata watu wa TRA waweza kukusanya kodi yao kwa ufanisi” alisema.
Meza kuu ilivyoonekana kabla ya kuzindua kituo hicho.
Alifafanua kuwa wawekezaji wa ndani ni vyema wakatumia kituo hicho vizuri kwa ajili ya uzalishaji wa viwanda vidogovidogo ili kuwezesha kuwainua wajasiriamali mbalimbali waliopo nchini.
Baadhi ya wafanyakazi wa kituo hicho walipokuwa wamekaa kumsikiliza mgeni rasmi.
Naye kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kituo Cha Uwekezaji (TIC), Cliffod Tandari alimhakikishia waziri kuwa malengo ya uzinduzi wa huduma mahala pamoja yatafanikiwa kwa kiasi kikubwa na kasi zaidi kama serikali ya awamu ya tano inavyoenda kwa kasi zaidi.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Waziri Charles Mwijage (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyikazi wa kituo hicho cha TIC.
Na Denis Mtima/Gpl
