The House of Favourite Newspapers

Yondani: Mtashangaa Kitakachowapata Waswana

NAHODHA msaidizi na beki wa kati tegemeo wa Yanga, Kelvin Yon­dani amesema wanataka kuwashangaza mashabiki wao kwa kuweka bonge la rekodi dhidi ya Town­ship Rollers ya Botswana.

Yanga, leo inatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Taifa wa Gaborone, Botswana kucheza na Rollers mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu hizo zinavaana katika mechi ya marudiano ya raun­di ya kwanza ya michuano hiyo baada ya mchezo uliopita Yanga kufungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Championi Jumamosi kutoka Botswana, Yondani alisema katika mechi hiyo watapambana kufa au kupona kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ya ushindi yatakayowavusha katika hatua inayofuata.

Yondani alisema, wana his­toria nzuri ya kupata matokeo mazuri ugenini kutokana na kucheza bila ya presha kama wanavyocheza mechi za nyum­bani, hivyo ana matumaini ya kupata ushindi .

“Kikubwa tunataka kuten­geneza historia ya kuwatoa Waswana ili tuwashangaze watu kwa sababu kila mtu anaamini kuwa tayari Yanga tumetolewa,” alisema Yondani na kuendelea.

“Kama umekuwa ukiifuatilia Yanga kwa ukaribu katika mechi za ugenini tumekuwa tukicheza kwa kiwango cha juu na kupata matokeo ma­zuri tofauti tukiwa nyumbani.

“Kwa upande wangu nimepanga kutimiza maju­kumu yangu vizuri pamoja na mabeki wenzangu kuhakiki­sha tunaokoa na kupunguza hatari langoni kwetu ili kuhak­ikisha haturuhusu bao.

Stori na Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Comments are closed.