The House of Favourite Newspapers

Vanessa Mdee, Millard Ayo, Wazidua Instagram Bure Ya Vodacom (Picha +Video)

Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma kwa Wateja, Linda Riwa (katikati) akiongea na wanahabari leo Mlimani City Jijini Dar. Mwanamuziki Vanessa Mdee akiendelea kumsikiliza Linda Riwa (kushoto).

 

KAMPUNI ya simu ya Vodacom leo imezindua rasmi huduma mpya ya kutumia Mtandao wa Kijamii wa Instagram bure nchini Tanzania kwa mara ya kwanza, uzinduzi uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.

 

Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma kwa Wateja, Linda Riwa amesema Vodacom ni mtandao pekee walioleta Instagram bure kupitia mtandao wa simu wa Vodacom. Wametambua kuwa wateja wao ni watumiaji wakubwa wa mtandao wa Instagram kutangaza bidhaa zao kwa kutuma picha na kusambaza ujumbe mbalimbali.

Wanahabari wakifanya yao wakati Linda Riwa akiongea.

Pia  akizungumza katika uzinduzi huo, Mtangazaji Millard Ayo, amewamasisha wateja wote wa Vodacom na watumiaji wa Mitandao huo wa Kijamii kuchangamkia fursa hiyo ambayo itarahisisha maisha kwani dunia ya leo kwa asilimia kubwa ipo mtandaoni.

 

Mwanamuziki Vanessa Mdee pia amewapongeza Vodacom kwa kuzindua huduma hiyo nzuri ambayo itamrahisishia yeye kama mwanamuziki kuwa karibu na mashabiki wake.

 

 

Ili kuweza kufaidika na huduma ya Instagram bure kutoka Vodacom, unachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi cha shilingi elfu moja na zaidi na kisha unajiunga na bando la Pindua Pindua.

 

Pata instagram BURE sasa kila unaponunua kifurushi cha Tshs 1,000 au zaidi usambaze na kuangalia picha BURE ukiwa kwenye mtandao supa pekee Tanzania , Piga *149*01# kujiunga.

Comments are closed.