The House of Favourite Newspapers

Mfaransa Aanza na Kichuya, Mavugo Simba

Shiza Kichuya.

KATIKA kukifanyia marekebisho madogomadogo kikosi chake, Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre, taratibu ameanza kumpumzisha kiungo wake, Shiza Kichuya na kutoa nafasi kwa wengine akiwemo Laudit Mavugo.

 

Kichuya tangu asa­jiliwe na Simba mwanzoni mwa msimu wa 2016/17, amekuwa akicheza dakika zote tisini na kuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo kupata matokeo ma­zuri kutokana na kufunga mabao na kutoa pasi za mabao.

Lakini hivi karibuni baada ya Lechantre kukabidhiwa mikoba Simba ameanza kumfanya mabadiliko Kichuya.

Wakati Kichuya akicheza muda wote, Mavugo mara nyingi amekuwa hana nafasi kikosini hapo hadi ikafikia hatua ya kutaka kuondolewa kwenye usajili uliopita wa dirisha dogo, lakini akabaki.

 

Taarifa kutoka kwenye benchi la ufundi la timu hiyo zinasema kuwa, Mfaransa huyo ameamua kufanya hivyo ili kutoa na­fasi kwa wachezaji wengine ambao awali hawakuwa wakipata nafasi licha ya kwamba wana uwezo wa kuipambania timu hiyo.

 

“Kocha anataka kuona kila mchezaji aliyekuwa kwenye kikosi chake anach­eza ndiyo maana amekuwa akifanya mabadiliko ya mara kwa mara ili kufaniki­sha malengo yake.

 

“Wapo wachezaji wale waliozoeleka kuwepo kwenye kikosi cha kwanza na wamekuwa wakicheza muda wote, yeye ameanza kuwapumzisha taratibu kama ilivyotokea kwa Ki­chuya, kisha kuwatumia wengine.

 

“Lakini pia, hata Mlipili (Yusuph) unavyomuona kwa sasa anacheza ni kuto­kana na kupewa nafasi na kuaminiwa, hivyo muda si mrefu utawaona wengine nao wakipewa nafasi,” alisema mtu huyo.

Kwenye mechi mbili za hivi karibuni za Simba ilipopambana na Al Masry kwenye Kombe la Shirikisho Afrika na kutupwa nje, hali hiyo ya mabadiliko ilijitoke­za kwa Kichuya.

Stori: Omary Mdose, D ar es Salaam

Comments are closed.