The House of Favourite Newspapers

Mfaransa Simba Awapigia Magoti Waamuzi

Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa, Pierre Lechantre (katikati).

KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Pierre Lechantre amefunguka kuwa amekuwa akipata wakati mgumu katika mechi za Ligi Kuu Bara zilizosalia kutokana na washambuliaji wake, tegemeo, John Bocco na Mganda, Emmanuel Okwi kukamiwa na mabeki wa timu pinzani.

 

Katika ligi hiyo, Simba kwa sasa inaongoza ikiwa na pointi 52, ambazo ni sita zaidi ya Yanga inay­oshika nafasi ya pili nyuma ya Azam inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 45.

Simba imefikisha pointi hizo baada ya juzi Jumatatu kufanikiwa kuifunga Mti­bwa Sugar bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

 

Akizungumza na Cham­pioni Jumatano, Lechantre amesema kuwa amekuwa akipata wakati mgumu kutokana na wachezaji hao kupata majeraha ya mara kwa mara kutokana na ku­kamiwa na mabeki wa timu pinzani jambo ambalo linaweza kuvuruga mipango yake ya ubingwa.

 

Kocha huyo amekwenda mbali zaidi kwa ku­waomba waamuzi kuongeza umakini wao kwa wachezaji wake hao ili waweze kufikia malengo ya msimu huu kwa kuwa safu ya ushambuliaji ndiyo tegemezi katika ufun­gaji wa mabao.

 

“Kiwango cha Bocco tangu atoke kwenye majeruhi kimezidi kupanda, amekuwa moto maana ukiangalia amesaidia kufunga ma­bao ya kutosha kwenye mechi za hivi karibuni.

 

“Lakini bado nimekuwa na hofu ya kuweza ku­maliza nao msimu wakiwa wazima kwa sababu, yeye na Okwi wamekuwa wakichezewa rafu kwa kuwa wana­kamiwa na mabeki wa timu pinzani kitu ambacho mara nyingi kinavuruga mipango yetu.

 

“Nadhani kuna haja ya waamuzi kuongeza umakini kwa sababu, soka siyo mchezo wa uadui lakini mabeki wa timu nyingi hufanya kusudi kabisa na ukiangalia ni wachezaji muhimu kwenye kikosi cha kwanza maana tunataka kushinda mechi zote,” alisema Lechantre.

Na Ibrahim Mussa na  Martha Mboma

Comments are closed.