The House of Favourite Newspapers

AJALI YA WANAFUNZI WA LUCKY VINCENT YATIMIZA MWAKA (Picha +Video)

Baadhi ya majeneza yenye miili ya wanafunzi 33, walimu wawili na dereva waliopoteza maisha wakati gari lilikokuwa limewachukua lilipopinduka eneo la Rhotia wilayani Karatu, mkoani Arusha.
Umati wa wakazi wa Jiji la Arusha na maeneo ya jirani ukiwa umefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid kuaga miili ya waliofariki katika ajali hiyo. 
Taaswira ya eneo la ajali hiyo.


Wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent jijini Arusha walipata  ajali  siku kama ya leo Mei 6 mwaka jana ambapo wanafunzi 33 wa darasa la saba, walimu wawili na dereva wa gari la shule hiyo walifariki dunia majira ya saa 3 asubuhi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Vifo hivi vilivyotikisa taifa vilishuhudia wanafunzi watatu kati ya wote wakipata majeraha na baadaye kupata matibabu huko Marekani ambapo walirejea na kuendelea na masomo kama kawaida.

Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi!

Eneo la Ajali ya Wanafunzi wa Lucky Vincent, Karatu


Shuhudia LIVE Watoto wa Lucky Vincent Walivyowasili Uwanja wa Ndege KIA

Comments are closed.