The House of Favourite Newspapers

KAMPENI YA  UJENZI OFISI ZA WALIMU DAR  YAFIKIA PAZURI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akitembelea baadhi ya ofisi za walimu zilizojengwa.

 

 

…Akizungumza jambo.

KAMPENI ya Ujenzi wa ofisi 402 za walimu wa Mkoa wa Dar es salaam imezidi kupamba moto ambapo baadhi ya ofisi hizo ujenzi wake umekamilika kwa kiasi kikubwa tayari kwa kukabidhiwa.

 

Akizungumza leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi huo kwa baadhi ya shule, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema miongoni mwa shule zilizokamilika ni Shule ya Kasulu Ilala, Shule ya Sekondari Makumbusho ambayo ilijengwa kwa ufadhili wa ubalozi wa China na waliojitolea kujenga shule tano kwenye wilaya zote za Dar es Salaam.

Makonda amesema ndani ya ofisi hizo kutakuwa na Ofisi ya mwalimu mkuu, mwalimu mkuu msaidizi, ofisi ya walimu wa kawaida, ukumbi wa mikutano, chumba cha kuhifadhi mitihani, vifaa vya michezo, chumba cha muhasibu, chumba cha kubadili nguo, mapokezi, bafu, vyoo safi, ofisi ya karani huku zikisheheni samani za kisasa.

Aidha  Makonda amesema mbali na kujenga ofisi za walimu pia atahakikisha shule zote za mkoa wake zinakuwa na umeme pamoja na maji ya kutosha kwani amepata wadau waliojitolea kuchimba visima 50 kwenye shule zenye uhitaji.

Comments are closed.