The House of Favourite Newspapers

Hizi Ndizo Nyimbo Alizosikiliza Meghan Siku Ya Ndoa

Meghan Markle akiwa na mume wake Prince Harry

MUIGIZAJI wa zamani wa Marekani, Meghan Markle ambaye kwa sasa ni mke wa Prince Harry ambaye ni mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, anadaiwa kusikiliza nyimbo za ‘Chill-out’, zilizotamba miaka ya 1950 wakati akiwa kwenye chumba akisubiri kwenda kanisani kufunga ndoa.

 

Kwa mujibu wa mtu wake wa karibu aliyekuwa naye kwenye chumba cha kujiandalia, anadai mwanadada huyo siku hiyo simu yake alitakiwa kuizima, ambapo kwa upande wa kujifurahisha aliomba awekewe nyimbo kupitia kwenye Mtandao a Spotify, za Chill Out.

 

“Simu yake alitakiwa kuizima. Alionekana mwenye shauku ya kila kilichokuwa kinaendelea, kwa hiyo ilibidi atafute namna ya kupotezea mawazo yake yote aliyokuwa anayawaza yatatokea,” alisema mtu huyo alipofanya mahojiano na Daily Mail.

Chill Out, ni ‘mix’ ya nyimbo mbalimbali za taratibu kutoka kwa wanamuziki mbalimbali, zimewekwa pamoja hasa kwa sababu ya watu wanaokuwa kwenye msongo wa mawazo, kusikiliza na kujiburudisha.

Hata hivyo mwanadada huyo siku ya leo, ametimiza wiki moja tangu Jumamosi iliyopita alipofunga ndoa.

 

Baada ya kuingia kwenye ukoo huo wa Kifalme na Malkia kuna baadhi ya vitu hataruhusiwa kuvifanya, ikiwa ni pamoja na kuigiza tena, kumiliki mtandao wa kijamii wa peke yake, kujihusisha na siasa, kusaini karatasi za mashabiki wake, kuvaa nguo fupi na kuonekana sehemu mbalimbali kiholela!

Comments are closed.