The House of Favourite Newspapers

Simba: Waliopo Kenya Ndiyo Watacheza Na Everton

Kikosi cha Simba kilichopo nchini Kenya kwenye mashindano SportPesa Super Cup.

 

UONGOZI wa Klabu ya Simba, umesema kuwa, wachezaji wao waliopo nchini hapa, ndiyo watapewa kipaumbele cha kwanza kucheza dhidi ya Everton endapo watafanikiwa kuwa mabingwa wa SportPesa Super Cup.

 

Katika michuano hiyo inayoendelea nchini hapa, Simba kesho Jumapili itacheza na Gor Mahia ambapo bingwa atakabidhiwa kombe na dola 30,000 pamoja na kupata nafasi ya kucheza mechi ya kirafiki na Everton katika Uwanja wa Goodison Park, England.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, alisema

vijana hao wakifanikiwa kubeba ubingwa huo, ndiyo watapewa nafasi hiyo kama shukrani kwao.

“Wachezaji tulionao hapa ndiyo wataenda kucheza na Everton kama tukifanikiwa kuwa mabingwa,

kama kutakuwa na ulazima wa kuwaongezea wengine tutafanya hivyo.

“Mbali na hilo, pia zawadi ya fedha tutawapatia wao wagawane kwa kuwashukuru kwa kuipa timu ubingwa huo,” alisema Manara.

Comments are closed.