The House of Favourite Newspapers

Tambwe: Yanga Wananidai, Ninabaki

Amissi Tambwe.

MSHAMB-ULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Amissi Tambwe raia wa Burundi ameibuka na kuweka wazi kwamba katika kipindi hiki cha usajili hana mpango wowote wa kuondoka ndani ya timu hiyo kutokana na kujiona ana deni la kulilipa baada ya kushindwa kuonyesha makali msimu uliopita.

 

Mshambuliaji huyo hakuwa na msimu mzuri katika msimu uliomalizika hivi karibuni baada ya kuandamwa na majeraha ya kila mara ya goti ambayo yalimsababisha kumaliza ligi akiwa hajafunga bao lolote lile.

 

Akizungumzia juu ya mustakabali wake ndani ya kikosi hicho, Tambwe ambaye yupo kwao kwa ajili ya mapumziko baada ya ligi kumalizika mshambuliaji huyo amesema hawezi kuondoka katika timu hiyo kwa sasa kufuatia kuvumiliwa kwa msimu mzima huku akiwa na majeraha ya mara kwa mara ambapo anataka kulipa fadhila kwenye msimu ujao.

 

“Kwa msimu uliopita sikuwa na kiwango kikubwa hivyo ninajiona kwamba nina deni la kulipa kwa Yanga ambao wamenivumilia licha ya kwamba nilikuwa na majeraha, ninachofanya sasa ni kujiandaa kwa ajili ya msimu ujao niwe vizuri,” alisema mshambuliaji huyo.

STORI NA SAID ALLY

Comments are closed.