The House of Favourite Newspapers

Aziz Ki: Malengo Yangu ni Ubingwa Kwanza, Mengine Baadaye

0

Kiungo wa Klabu ya Young Africans, Stephane Aziz Ki, amebainisha kwamba, malengo yake ya kwanza msimu huu ni kuona anaisidia timu yake hiyo kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.

Aziz Ki ambaye ndiye kinara wa magoli katika ligi hiyo msimu huu akifunga 15, amesema baada ya lengo la kwanza kutimia, ndipo atafikiria Tuzo ya Ufungaji Bora.

“Lengo langu namba moja msimu huu ni kubeba ubingwa na sio kutwaa Kiatu cha Ufungaji Bora, ishu ya ufungaji bora itakuja baada ya kushinda ubingwa,” alisema Aziz Ki.

Aziz Ki ambaye huu ni msimu wa pili akiitumikia Young Africans, amehusika kwenye jumla ya magoli 22 kati ya 54 yalifungwa na timu yetu katika ligi, amefunga 15 na asisti 7.

Leave A Reply