The House of Favourite Newspapers

TAASISI YA WAZALENDO NA NGUVU YA MWANAMKE WAADHIMISHA ‘SIKU YA MTOTO WA AFRIKA’

Mgeni rasmi katika hafla hiyo Bi. Kate Kamba akizungumza na watoto, wanafunzi, walimu na wadau wengine.

TAASISI ya Wazalendo Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Nguvu ya Mwanamke leo wameadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Lamada Jijini Dar.

Akizungumza na Global TV, Mwenyekiti wa Mzalendo Tanzania, Allein Sethi, amesema maadhimisho hayo ambayo hufanyika Barani Afrika Juni 16 kila mwaka, mwaka huu walishindwa kuyaadhimisha siku hiyo kutokana tarehe hiyo kuangukia Sikukuu ya Iddi Pili siku ambayo ingekuwa vigumu kujumuika na watoto hao.

Katika hafla hiyo walialikwa watoto, wanafunzi kutoka shule mbalimbali, walimu, wadau wa usalama barabarani na viongozi wa kisiasa ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Kate Kamba.

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL

 

 

 

Comments are closed.