The House of Favourite Newspapers

Ukikatwa Usianze Nongwa Tulia

0

UKIKATWA USIANZE NONGWA TULIA

 

Katibu mkuu wa Jumuiya ya wazazi CCM Taifa Comred Ally Salum Hapi amewatahadharisha watu wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali katika chaguzi zijazo kupitia chama cha mapinduzi hususani katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani 2025 kuelewa namna mchakato wa kupata wagombea unavyokuwa kwani kwa mujibu wa katiba kila mwanachama mwenye sifa anaruhusiwa kugombea nafasi yoyote,lakini inapofika kwenye uteuzi si kila mtu atateuliwa wapo watakaoachwa ukiachwa tulia.

 

Hapi amesema hayo wakati akizungumza viongozi wa chama,jumuiya na wilaya ya Chemba mkoa wa Dodoma baada ya kuwasili kwa ziara ya siku tatu katika mkoa huo Hapi pamoja na kueleza malengo ya ziara hiyo lakini akatumia nafasi hiyo kufikisha ujumbe kwa wanachama wa ccm wanaojipanga kugombea nafasi za uongozi kupitia chama hicho.

 

“Kama mnavyojua mwaka huu tuna uchaguzi wa serikali za mitaa kwetu kama chama ni uchaguzi muhimu kuwapata viongozi bora wanaotokana na ccm,wanaokubalika na wananchi na wanaoweza kukifanya chama chetu kiendelee kuwa imara na mwisho tupate ushindi katika uchaguzi mkuu mwakani”

 

“Hatuwezi kushinda tu uchaguzi kwa miujiza tunatakiwa kujipanga kuanzia sasa lakini pia tupate wagombe makini wanaoweza kupeperusha bendera ya ccm bila mashaka kwakuwa wanatikana na wananchi hivyo niwaombe sana viongizi wenzangu tujiandae kuhakikisha chama chetu kinapata ushindi na hatuna mashaka kwa kazi kubwa iliyofanya na mwenyekiti wetu wa chama na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Haitii Shaka hata kidogo”alisema hapi

Kuhusu wagonbea wanaotafuta uongozi amewataka kujua misingi ya kupata wagombe katika chama kujua kwamba zipo hatua za uteuzi wa wagombea kwahiyo inapotokea mwanaccm hajateuliwa amewataka kuwa watulivu badala ya kuanza nongwa,chokochoko na kutengeneza makundi hivyo amewataka kusimama na kuendelea kuunga mkono wagombea watakaoteuliwa kwani ushindi wao ni wa CCM.

“wapo baadhi yetu ambao hudhani kuwa lazima wateuliwa na wagombee nafasi za uongozi na wasipoteuliwa huanza nongwa na kutafuta nani mchawi,mimi nataka niwambie inapotokea hujateuliwa tulia usilete nongwa kanakwamba ilikuwa lazima uwe wewe hapana wakati wako haujafika ndiyo maana hujapata na pengine Mwenyezi mungu amekuepusha na vitu fulani kwenye hiyo nafasi kwahiyo tulia”alisema Hapi

Lakini pia hapi chama cha mapinduzi ndiyo chama kilichojipanga kuongoza nchi kutokana na mipango na misingi iliyopo kuanzia ngazi ya chini kwenye vitingoji tofauti na vyama vingine huku pia akieleza namna CCM inavyotumia ilani kunadi sera zake hiyo inaashiria kuwa chama kinamfumo wa kutambua kero za wananchi na mahitaji yao.

Leave A Reply