The House of Favourite Newspapers

Singano Aitaka Jezi ya Chirwa Yanga

Ramadhan Singano ‘Messi’

WINGA wa Azam FC ambaye kwa mujibu wa mashabiki alipotea kwenye ramani baada ya kutoka Simba, Ramadhan Singano ‘Messi’ amesema yupo tayari kuvaa jezi ya Obrey Chirwa pale Yanga ikiwa klabu hiyo itafuata utaratibu wa kumsajili.

 

Yanga kwa sasa wanasaka mbadala wa Chirwa ambaye amemaliza mkataba kikosini humo ambapo sasa inadaiwa staa huyo amejiunga na Klabu ya Ismailia ya Misri.

Singano alianza kuhusishwa kujiunga na Yanga mara baada ya winga wake, Simon Msuva kuondoka kikosini humo na kutua Difaa El Jadida kwa dau la Sh mil 335.9.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Singano alisema mpaka sasa bado ana mkataba na Azam FC lakini kama Yanga watakwenda na kuzungumza nao kisha wakakubaliana basi yeye atakuwa tayari kwenda kuvaa jezi ya Chirwa.

Ramadhan Singano ‘Messi’

Staa huyo aliyewahi kuichezea Simba kabla ya kutua Azam, aliongeza kuwa; “Binafsi bado nina mkataba na Azam, kuhusu kwenda Yanga kiukweli habari hizo hata mimi ninazisikia lakini wao hawajanifuata rasmi lakini kama wakiwafuata Azam na kuzungumza nao na kukubaliana kisha waongee na mimi hiyo haina tatizo.”

 

“Yanga wanakaribishwa kikubwa ni makubaliano, mimi ni mchezaji nipo tayari kucheza sehemu yoyote lakini lazima tukubaliane kwanza na timu yangu pili na mimi mwenyewe niridhie, vitu kama hivi wanafanya hadi Ulaya,” alisema Singano ambaye ni miongoni mwa wachezaji wanaoishi maisha mazuri ya wastani Jijini Dar es Salaam kutokana na kinachoingia kwenye akaunti yake.

Comments are closed.