The House of Favourite Newspapers

Okwi, Bocco Kuanza Kazi Simba Wiki Ijayo

ACHANA na maujuzi ya Meddie Kagere ‘Medi Magoli’, Marcel Kaheza, Adam Salamba au Mohamed Rashid. Yale makali yao waliyoonyesha kwenye Kagame na kuwafurahisha mashabiki wa Msimbazi achana nayo, sahau kabisa.

 

Sasa goma linaanza upya, yaani ndio kwanza kumepambazuka. Wenye timu yao ambao ni Shiza Kichuya, Emmanuel Okwi na John Bocco wanajiunga na wenzao wiki ijayo tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu.

Simba iliwapa mapumziko baadhi ya nyota wake wakiwemo Okwi na Bocco pamoja na Haruna Niy­onzima, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Kichuya na Shomari Kapombe baada ya kuwa­tumia kwenye michuano ya SportPesa isipokuwa Okwi na Bocco.

 

Kocha wa timu hiyo, Masoud Djuma alisema ; “Wachezaji wetu wale ambao wa­likuwa kwenye mapumziko wataungana na wenzako mara baada ya michuano ya Kag­ame kumalizika sababu michuano ikimal­izika watapewa mapumziko kama siku nne hivi baada ya hapo ndipo wote wataweza kuungana na kuanza maandalizi.”

Comments are closed.