The House of Favourite Newspapers

Mourinho Amkatia Tamaa Sanchez

Msham­buliaji Alexis Sanchez

KOCHA Jose Mour­inho amekiri kuwa kumkosa msham­buliaji wake, Alexis Sanchez kwa siku 20 ni pigo kubwa katika kikosi chake wakati huu ambapo kipo kwenye ziara nchini Marekani.

 

Sanchez alizuiliwa kuingia nchini humo akiwa na kikosi cha Manchester United kutokana na tatizo la Visa lililotokana na rekodi za nyu­ma za mche­zaji huyo kutolipa kodi miaka ya nyuma akiwa nchini Hispania.

 

Mourinho amekiri kuwa kuto­kuwa na staa huyo ambaye pia alikuwa katika mapumziko ya muda mrefu kwa kukosa kushiriki michuano ya Kombe la Dunia kuna mpa hofu juu ya ufiti wake.

 

“Sijui kama ataweza kujiunga na sisi, hii ni habari mbaya kwetu, kwake na kwa timu kwa jumla, hata kwa waratibu wa michuano ya huku (Marekani) siyo nzuri.

 

“Lakini hakuna wa kumlaumu, klabu inafanya kazi kubwa na nina heshimu mamlaka za Marekani na litakuwa jambo la muhimu kufanya kazi na (Anthony) Martial, Alexis na (Juan) Mata ambao ni wachezaji tulionao kwenye idara ya ushambuliaji.

 

“Hatuna (Romelu) Lukaku, (Jesse) Lin­gard, Marcus Rash­ford, ndiyo maana nasema Alexis akiko­sekana kwa siku 20 ni jambo bay asana,” al­isema kocha huyo.

RATIBA YA ZIARA YA MAN UNIT­ED

Julai 20 – Club America

Julai 22 – San Jose Earthquakes

Julai 25 – AC Milan

Julai 28 – Liverpool

Julai 30 – Real Madrid

Comments are closed.