The House of Favourite Newspapers

WASTARA AMSHUKURU MAGUFULI KUSAIDIA MATIBABU YAKE

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Msanii wa Filamu nchini, Wastara Juma alipofika ofisini kwake jana jijini Dodoma kwa ajili ya kumshukuru Rais John Magufuli na serikali kwa michango waliyotoa kufanikisha matibabu yake  nchini India katika hospitali ya Saifee.

Msanii wa Filamu Bongo, Wastara Juma,  jana alifika katika ofisi za Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe jijini Dodoma kumshuruku Rais John Magufuli kwa msaada aliompa kufanikisha matibabu yake ya mguu nchini India katika hospitali ya Saifee Februari mwaka huu ambapo alisema sasa afya yake imeimarika.

Comments are closed.