The House of Favourite Newspapers

DULLAH MBABE AMTWANGA SAIDI MBELWA DAR LIVE

Mwamuzi  Pembe Ndava akisubiri (katikati) kumtangaza mshindi mara baada ya kumalizika kwa pambano kati Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ (wa pili kushoto) na Saidi Mbwela ‘Moto wa gesi’  katika ukumbi wa Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Dulla Mbabe akilia kwa furaha mara baada ya kutangazwa mshindi.
Mashabiki wakimpongeza.
…Akipewa huduma ya kwanza baada ya pambano kutokana kupata maumivu ya bega.
…Akimrushia makonde mazito Mbelwa.
…Akiendelea kumdhibiti Mbelwa.
Mbelwa akionekana kuwa na nguvu mpya. 
Mashabiki waliojitokeza kushuhudia mpambano huo.
Mbelwa akirusha konde. 
Tahadhari ya kupiga na kupigwa.
Promota Diego akiongea na mashabiki kabla ya shindano.

Dullah  na wapambe akipanda ulingoni kabla ya pambano.

Mbelwa  akiwa amebebwa na wapambe kuelekea ulingoni.

BONDIA wa  kulipwa,  Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’,  amefanikiwa kumchakaza vikali mpinzani wake,  Saidi Mbelwa ‘Moto wa Gesi’.  katika pambano la kumaliza ubishi lililofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa Dar Live,  uliopo Mbagala Zakhem,jijini Dar es Salaam.

 

Katika pambano hilo ambalo lilikuwa la kumaliza ubishi kati ya mabondia ambapo Mbabe alifanikiwa kuongoza raundi nyingi licha ya kuumia bega la mkono wake wa kushoto lakini alifanikiwa kumuangusha mpinzani wake mara mbili katika raundi ya tatu na ya nne.

 

Kabla ya pambano hilo kubwa waliweza kushuhudia mapambano ya utangulizi huku lililovutia zaidi ni pambano la  wadada  kati ya Maimuna Hashimu na Happy Daudi ambalo lilimalizika kwa Happy Daudi kushinda kwa pointi .

Mapambano mengine ya utanguliza yalikuwa kati Paulo Kamata na Shabani Kaoneka na Paulo kamata akiibuka mshindihuku Saidi Wigo akipigwa na Faraji  Sayuni kwa pointi.

 

PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL

 

Comments are closed.