The House of Favourite Newspapers

Mambo Yanoga Maadhimisho Miaka 20 Ya Twanga Pepeta

Baadhi ya wanakamati wakimsikiliza Mkurugenzi wa Twanga, Asha Baraka.

MAMBO yanazidi kunoga katika maandalizi ya maadhimisho ya Miaka Ishirini ya Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ ambayo yanatarajiwa kufanyika mwezi ujao, kwenye Ukumbi wa The Legends Club, uliopo Namanga, Dar.

 

Siku ya jana kikao cha kamati ya maadhimisho hayo ilikutana kwenye ukumbi huo, ili kupanga namna ambavyo mambo yatakuwa.

Mwanamuziki wa Twanga, Kalala Junior akizungumza jambo kwenye kikao hicho, (katikati) ni mmoja wa wanakamati na (kulia) ni Luiza Mbutu, mwanamuziki mkongwe wa Twanga.

Kabla ya kufikia siku hiyo, Twanga na wadau wake wanatarajia kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea hospitali mbalimbali, kutoa misaada kwenye vituo vya wahitaji wakiwemo watoto yatima na mambo mengine mengi.

 

Lakini pia kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Twanga Pepeta, Asha Baraka alisema watafanya pia dua kwa ajili ya marehemu wote ambao walipita kwenye bendi hiyo kama ishara ya kuwakumbuka.

 

Baadhi ya marehemu hao ni Abuu Semhando, Ismail Kizunga, MCD, Banza Stone, Joseph Watuguru, Halima White, Happy Choki, Diana Aston Villa, Pendo Bouda, Mwantumu MCD na Amigo Rasi.

 

Katika maadhimisho hayo mpango mzima wa burudani kwa upande wa Twanga utaongozwa na wanamuziki wakali, Kalala Junior pamoja na Luiza Mbutu.

Baadhi ya wanakamati wakifuatilia kikao hicho.

 

Lakini pia bendi mbalimbali zimealikwa na Twanga inaendelea kupokea mrejesho juu ya bendi zitakazoshiriki.

Stori: Boniphace Ngumije

Comments are closed.