The House of Favourite Newspapers

Zahera Bado Hajaridhishwa Na Kiwango Cha Yanga

LICHA ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kuwa bado hajaridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na nyota wake.

 

Katika mchezo huo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu huu uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga ilipata ushindi huo kupitia mabao ya Heritier Makambo na Kelvin Yondani, huku Haruna Chanongo akiifungia Mtibwa Sugar bao la kufutia machozi.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Zahera raia wa DR Congo na Ufaransa, alisema; “Bado kuna tatizo kwenye kikosi changu, kwa sasa ukiangalia wachezaji wangu wengi hawapo fiti kwa asilimia mia moja, wengi wamefikisha asilimia 70, Makambo peke yake ndiye naweza kusema amekamilika kwa asilimia mia.”

 

“Tuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha makosa haya hayajirudii tena, lakini pia ni lazima wachezaji wengine nao

 

wanatakiwa kuwa fiti kama Makambo,” alisema Zahera ambaye kutokamilika kwa kibali chake cha kazi kumeibua mijadala.

 

Kuhusu ishu ya kibali cha kufanyia kazi kwa kocha huyo, Katibu wa Yanga, Omary Kaaya alisema kwa sasa wanaangalia zaidi namna gani timu inapata matokeo bila kocha kuwepo kwenye benchi.

Comments are closed.