The House of Favourite Newspapers

KIMENUKA! MAMA AANIKA MAPYA YA MCHUMBA WA WEMA

DAR ES SALAAM: Baada ya uvumi wa bintiye kupata mchumba na kwamba anatarajia kuolewa na jamaa anayefahamika kwa jina la R.a.h.u.r kushika kasi, mama wa muigizaji Wema Sepetu, Miriam Sepetu ameibuka na kuanika mapya kuhusu ishu hiyo.

Siku za hivi karibuni, kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram, kurasa mbalimbali zimekuwa zikipamba na picha ya Wema na R.a.h.u.r huku wakisindikiza na jumbe zinazoashiria kwamba mipango ya ndoa ya wawili hao inafanyika na inakwenda vizuri.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, mama huyo alisema kwanza hamtambui mwanaume huyo anayetajwa kuwa mchumba wa Wema na amekuwa akiona vitu hivyo vikizushwa tu mitandaoni.

Alisema kuwa, kama kweli kungekuwa na mchumba anayetaka kumuoa mwanaye basi kama mama, asingesikia kwenye mitandao bali angemuona nyumbani kwake na kueleza dhumuni lake hilo kwa maandishi.

 

“Mimi sitambui kabisa kama kuna mchumba eti ambaye ameshakuja kwangu na amemposa mtoto wangu na tayari tuko kwenye taratibu za ndoa hiyo sio kweli kabisa wala hakuna kitu kama hicho maana mimi ndio mzazi mwenyewe,” alisema mama huyo.

 

Aidha, mama huyo aliongeza kuwa watu waache kusikiliza mambo ya mtandaoni kwani mengi ni ya kizushi na kama mtu akitaka kuujua ukweli kumhusu yeye au mwanaye ni vyema wakamtafuta yeye au bintiye.

“Watu wasikazanie kuamini vitu vya mtandaoni kabisa kwa sababu vitu vingi sio vya kweli kabisa na mtandaoni kunapotosha sana ni bora kupata ukweli wa jambo lolote kutoka kwa mhusika mwenyewe,” alisema mama huyo.

 STORI: IMELDA MTEMA, IJUMAA

 

MAUMIVU: Mume Alia KUPORWA Mke/KIGOGO MZITO Ahusishwa

Comments are closed.