The House of Favourite Newspapers

GARI LA WATALII LAGONGANA NA LORI ARUSHA

Taswira ya eneo la ajali kati ya lori na gari dogo lililokuwa na watalii.

 

Gari ya watalii imepata ajali mbaya Jijini Arusha.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (SACP) Ramadhani Ng’anzi, amethibitisha kutokea kwa ajali ya gari iliyohusisha Lori na gari ya kubeba watalii.

 

Ajali hiyo imetokea eneo la Mti mmoja Wilayani Monduli.

 

Kamanda Ng’anzi amesema gari aina ya Land Cruiser iliyokuwa imebeba watalii imegongana uso kwa uso na Lori la mizigo takribani Kilometa 10 kutoka njia panda ya Monduli.

 

”Nipo eneo la ajali hapa muda huu, tunaendelea na vipimo hapa, nitawajulisha kwa undani lakini vifo vipo ila bado hatujajua ni idadi gani”, amesema.

Taarifa za awali zinaeleza takribani watu watano wamefariki katika ajali hiyo.

 

Gari lililobeba watalii baada ya ajali. 

Comments are closed.