The House of Favourite Newspapers

Waziri Mavunde azindua Muonekano Mpya wa Chupa ya K-Vant

Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde akizungumza jambo  kwa wadau  mbalimbali  wa Kinywaji cha K-VANT  wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa. 
Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde (wapilikulia) akionyeshwa na Meneja mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mega Beverages , Marco Maduhu Chupa  mpya ya K-Vant  wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa ya kinywaji cha K-Vant uliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Francis Kimaro.
Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde (kulia)  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Mega Beverages, wazalishaji wa Kinywaji cha K-Vant ,Francis Kimaro (kushoto) na Meneja mauzo na Masoko wa Kampuni hiyo Marco Maduhu, wakigongeana glasi ya K-VANT wakati wa uzinduzi wa Chupa  mpya ya K-Vant.  
Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde (katikati) Mkurugenzi wa uzalishaji wa kinywaji cha K-VANT ,Cuthbert Sawe (kushoto)  na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mega Beverages Francis Kimaro , wakionja radha ya kinywaji cha K-VANT. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Kamapuni ya Mega Beverages wazalishaji wa kinywaji cha K-VANT  wakigongesha glasi na Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde,  wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa kinywaji cha K-VANT waliohudhulia kwenye uzinduzi wa muonekano mpywa wa chapa ya kinywaji hicho. 
Baadhi ya wadau mbalimbali wa kinywaji cha K-VANT waliohudhulia kwenye uzinduzi wa muonekano mpywa wa chapa ya kinywaji hicho. 
Waziri Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa Kampuni ya Mega Beverage Company Limited, ya mkoani Arusha.

 

Kampuni ya Mega Beverage Company Limited,ya mkoani Arusha, inayotengeneza pombe kali  chapa maarufu ya K Vant, imezindua chupa mpya za kinywaji cha K-Vant zenye mwonekano tofauti na chupa za awali.Mabadiliko hayo hayakubadilisha ladha  halisi ya kinywaji hicho na wateja wake wataendelea kuifuahia ikiwa katika ladha yake halisi ya siku zote.

 

Lengo kubwa la kubadilisha chupa za pombe ya K-Vant, ni mkakati wa kampuni wa kupanua masoko yake ya ndani na nje ambapo imelenga kuwa katika mwonekano bora zaidi bila kuathiri ladha halisi ya kinywaji hicho ambayo inapendwa na watumiaji wengi wa pombe kali nchini na nje ya mipaka ya Tanzania.

 

 

Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Antony Mavunde.

 

 

Mh.Mavunde,alipongeza  hatua ya kampuni kubuni mkakati wa kuongea soko la bidhaa  na kuongeza kuwa masoko yakiongezeka ndivyo mapato ya serikali yanaongezeka kupitia kulipa kodi sambamba na kuongeza wigo wa  ajira kutokana na kuhitajika nguvu kazi zaidi.

 

“Serikali ya awamu ya tano  inao mkakati wa kuifanya Tanzania nchi ya viwanda, tutazidi kuboresha mazingira zaidi kwa wawekezaji katika sekta hii ili lengo la kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta hii lifanikiwe  haraka  sambamba na kupunguza changamoto ya tatizo la ajira kwa vijana “,alisema.

 

 

Mkurugenzi wa Masoko wa Mega Beverage Company Limited,Marco Maduhu alisema, “Kauli mbiu yetu ya  kinywaji cha K-Vant katika mwonekano mpya ni ’Ni Halali Yako’    kampuni imejipanga  kuimarisha usambazaji wa bidhaa ya pombe ya K-Vant  katika sehemu zote nchini ili watanzania waendelee kufurahia ubora wake kikiwa katika mwonekano wa chupa mpya  na katika ladha ileile waliyoizoe kuipata  siku zote,”.

 

 

Alisema uzinduzi wa chupa mpya za K-Vant mbali na kufanyika katika mkoa wa Dar es Salaam pia utafanyika katika mikoa ya Arusha na Mwanza, pia usambazaji wa kinywaji hiki kwenye mwonekano mpya katika ladha yake halisi utaendelea kufanyika katika mikoa yote nchini  kuanzia sasa.”Wateja wetu wowote popote mlipo tunawashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono nasi tutaendelea kuboresha huduma zetu za usambazaji na  kuhakikisha kinywaji  bora cha K-Vant kinawafikia popote mlipo kikiwa katika chupa mpya,”alisisitiza.

 

 

Maduhu alioongeza  kuwa, kampuni ya Mega Beverage itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ambapo kupitia uwekezaji wake itahakikisha inaendelea kuchangia pato la taifa kupitia kulipia kodi mbalimbali, kunufaisha watanzania wengi kupata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, pia imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali kwenye jamii.

 

Comments are closed.