The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Aongoza Sherehe Za Maadhimisho Ya Miaka 60 Ya Muungano, Uwanja Wa Uhuru, Dar – (Picha +Video)

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wananchi pamoja na Viongozi mbalimbali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024.
Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakiwa kwenye kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024.
Gwaride la Heshima la Miaka 60 ya Muungano lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Viongozi mbalimbali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki maadhimisho ya kiaka 60 ya Muungano leo tarehe 26 Aprili, 2024 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2024.
Rais Samia akiwa amesimama wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania na ule wa Afrika Mashariki ukiimbwa katika Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Rais Samia akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kushuka kwenye gari Maalum la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Rais Samia akikagua Gwaride la Heshima.

Leave A Reply